25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Solskjaer: Barcelona wapewe tu taji la UEFA

BARCELONA, HISPANIA

BAADA ya Manchester United kukubali kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona, kocha wa timu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer, ameweka wazi kuwa wapinzani hao watachukua taji hilo msimu huu.

Barcelona walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani Camp Nou na kufanikiwa kushinda mabao 3-0, huku Lionel Messi akifunga mabao mawili na bao jingine likifungwa na Philippe Coutinho na kuwafanya wasonge mbele hatua ya nusu fainali.

Mchezo huo ulikuwa wa robo fainali ya pili, wakati huo mchezo wa kwanza ulipigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford na Manchester United kukubali kichapo cha bao 1-0, hivyo Barcelona wameingia nusu fainali kwa ushindi wa jumla mabao 4-0.

Baada ya kumalizika kwa mchezo wa juzi, kocha huyo aliulizwa nafasi ya Barcelona kwenye michuano hiyo anaionaje? Alijibu: “Ninaamini Barcelona wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

“Kutokana na ubora walionao katika safu ya ushambuliaji, wana nafasi kubwa sana, kuna wachezaji wengine wa timu hiyo ambao wana uwezo mkubwa kama vile Ousmane Dembele na Malcom.

“Hivyo, kwa upande wangu ninasema kuwa Barcelona wanakwenda kutwaa ubingwa msimu huu, japokuwa ushindani ni mkubwa kwa hatua waliofikia, lakini wana nafasi kubwa sana,” alisema kocha huyo.

Kwa sasa Manchester United wanakwenda kuzihamishia nguvu zao kwenye michuano ya Ligi Kuu England ili kuona uwezekano wa kuingia katika nafasi nne za juu ili waweze kushiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao, kwa sasa wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi.

Mchezo mwingine ambao ulipigwa juzi ni pamoja na Juventus ambao walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani na kukubali kufungashiwa virago dhidi ya Ajax huku Juventus wakikubali kichapo cha mabao 2-1.

Mchezo wa kwanza ambao Ajax walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani wiki iliyopita, ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, hivyo juzi Juventus walishindwa kutamba nyumbani kwao.

Ajax msimu huu wanaonekana kuwa bora kwa kuwa walinzi kwa kuwatoa mabingwa watetezi Real Madrid katika hatua ya 16 bora na sasa wamefanya hivyo kwa kukiondoa kikosi kinachoongozwa na mshambuliaji hatari, Cristiano Ronaldo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles