Kampuni zilizoiingia mikataba na Kanumba, Majuto kuzilipa familia zao

Mwandishi Wetu

Kampuni ya Steps Entertainment imeshamkabidhi Mama wa  muigizaji marehemu, Steven Kanumba malipo ya ziada ya Sh milioni 15 baada ya kugundulika kuwa iliingia mkataba mbovu na msanii huyo.

Pia kampuni hiyo imeahidi kushirikiana na mama yake Marehemu Kanumba, kuandaa filamu ya maisha ya mwanawe huyo.

Taarifa hiyo ilitolewa bungeni leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, alipokuwa akiwasilisha makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20.

 Waziri Mwakyembe amesema Pamoja na malipo hayo Kampuni ya Pan African Enterprises Ltd na Ivori Iringa, zimeshaingiza kwenye akaunti maalum Sh milioni 30 kwa kazi alizotekeleza muigizaji marehemu Amri Athuman maarufu King Majuto.

“ Lakini pia Kampuni ya Azam SSB imeandaa malipo ya ziada ya sh milioni 20 na Kampuni ya Tanfoam ya Arusha imeandaa Sh milioni 15 yatakayowasilishwa kwa msimamizi wa mirathi ya marehemu King Majuto,”amesema Mwakyembe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here