24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Zitto, Mbowe waishutumu Ofisi ya DPP

Na Mwandishi Wetu

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo), ameishutumu Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DPP), kwamba imekuwa na utaratibu wa kukubaliana na wahalifu na kuwatoza faini ili makosa yao yafutwe hata kama wana mashtaka mahakamani.

Kutokana na hali hiyo, ameitaka Serikali itoe ufafanuzi ni kwanini ofisi hiyo inakubaliana na wahalifu hao.

Zitto ameyasema hayo bungeni leo Ijumaa Aprili 12, alipokuwa akichangia makadirio ya bajeti ya Wizara ya Tamisemi, Utawala Bora pamoja Utumishi wa Umma.

Akitoa mfano Zitto amesema kesi za watumishi wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, ambapo watumishi wake waliokuwa na kesi mahakamani kwa kosa la utakatishaji fedha waliachiwa baada ya mazungumzo kufanyika.

Wakati Zitto akisema hayo, Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (Chadema), amesema utaratibu huo wa Ofisi ya DPP kukubaliana na watuhumiwa unawatisha wawekezaji kwa kuwa haufuati utawala bora.

Katika maelezo yake, Mbowe alitolea mfano Mbia wa serikali katika mradi wa mabasi ya mwendokasi jijini Dar es Salaam, Simon Kisena ambaye ana kesi mahakamani.

Kwa mujibu wa Mbowe serikali ingeweza kuzungumza na Kisena na kumaliza tofauti zilizopo kwa vile wana ubia katika mabasi hayo.

Wakati huo huo, Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM), aliitaka ofisi hiyo ya DPP iwe na utaratibu wa kuwaachia watuhumiwa wasiokuwa na makosa badala ya kuendelea kuwashikilia bila sababu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles