23.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Zawadi ya ‘Birthday’ yampoza Mtumishi wa serikali Liberia

Monrovia ,Liberia

Wanachama vijana wa chama tawala (Congress for Democratic Change) nchini Liberia wamelaani kitendo cha mtumishi wa serikali kutoka ofisi ya rais kuonekana katika video akimzawadia mke wake gari la gharama katika siku yake ya kuzaliwa huku akilimwagia shampeni.

Vijana wa chama hicho tawala wameeleza kitendo alichokifanya James Emmanuel Potter wiki iliyopita ni kwenda kinyume na kanuni, itikadi tokea kuanzishwa kwa chama hicho.

Wafuasi hao wanamshutumu mtumishi huyo wa serikali ambaye ni msimamizi wa vifaa katika ofisi ya urais kwa kutojali uhalisi wa wakati huo, katika moja wa nchi masikini zaidi Afrika.

Hata hivyo kiongozi huyo kupitia moja ya ukurasa wake wa mtandao wa kijamii amesema kuwa anafanya kazi ili kupata mshahara wa kumuwezesha kupata chochote kitakachompendeza.

Mmoja wa mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa facebook alinukuliwa kwa kumkosoa naibu waziri wan chi hiyo na kuandika kuwa Potter, kumnunulia mke wake gari aina ya Audi SUV na kumwaga shampeni ya gharama wakati wananchi wanaangaika na maisha, Je huyu ni maskini?”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,244FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles