25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Zantel yazindua ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Kampuni ya simu ya Zantel leo Machi 16, 2021 imezindua kampeni yake mpya ijulikanayo kama ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’ inayolenga kuwaelimisha wateja juu ya uhumimu wa mtandao wa 4G katika kujiletea maendeleo.

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatano Machi 17, 2021 katika viwanja vya Kisonge mjini Unguja ambapo wananchi wameweza kushiriki na kujionea ni namna gani wanaweza kutumia mtandao wa 4G kwa manufaa ya kijamii na kiuchumi.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Wizara ya Mawasiliano Zanzibar, Dk. Mzee Suleiman Mndewa (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Pasua Anga Ki Zantel 4G uliofanyika kupitia televisheni ya ZBC. Kulia ni Mkuu wa Zantel Zanzibar Mohammed Khamis Mussa pamoja na Zuena Ali (mjasiriamali). Kampeni hiyo imelenga kuelimisha umma juu ya umuhimu wa matumizi ya mtandao wa 4G katika kujiletea maendeleo.

Kabla ya uzinduzi huo, Kampuni ya Zantel iliendesha mjadala ulijadili juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G ambao uliruka kupitia televisheni ya ZBC.Mdahalo huo ulihusisha wadau mbalimbali kutoka Serikalini pamoja na wajasiriamali.

Akizungumza wakati wa mjadala huo, Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa, amesema; “Nia yetu ni kunaendelea kuboresha mtandao wetu ili mawasiliano yapatikane Zanzibar yote kwa kasi ya 4G kumuwezesha mtumiaji kuweza kufanya mawasiliano bora na ya haraka. Na sasa tunazindua kampeni ya PASUA ANGA ki ZANTEL 4G mahsusi ili kutoa elimu kwa umma juu ya manufaa mbalimbali ya mtandao ulioboreshwa wa Zantel 4G,” amesema.

Katika uzinduzi uliofanyika viwanja vya kisonge, ulihusisha shughuli mbalimbali ikiwamo michezo ya foosball, tebal tennis, pool table huku washindi wakiibuka na vifurushi vya intaneti ya 4G vya wiki pamoja na zawadi mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles