23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Zabibu huliongezea ini uwezo wa kuondosha sumu mwilini

ZABIBUU

NA MWANDISHI WETU,

ZABIBU hujulikana kama chanzo kizuri cha divai, lakini pia huweza kuliwa kama tunda.

Matunda haya inaelezwa kwamba yalianza kulimwa nchini Uturuki wakati kwa hapa nyumbani yakipatikana zaidi katika Mkoa wa Dodoma.

Matunda haya yana rangi mbalimbali ambazo ni nyekundu iliyoiva, nyeusi, bluu ya kukoza, njano, kijani na hata pinki, licha ya kwamba kwa Tanzania yanapatikana zaidi yenye rangi nyeusi.

Zabibu ni moja ya tunda lenye sifa nyingi kutokana na uwezo wake wa kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hususani ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo.

Faida zake 

Tunaelezwa na wataalamu kuwa zabibu husaidia damu kuwa nyepesi na kuifanya isigande ndani ya mishipa ya damu, hivyo mtumiaji wa zabibu hupunguza hatari ya kupata kiharusi (stroke).

Tunda hili pia husifika kwa kutibu tatizo la upungufu wa damu, hususani kwa wale wanaotumia mara kwa mara kwani huwasaidia kuepukana na ugonjwa wa bawasili pia.

Pia husaidia katika tiba na kinga dhidi ya magonjwa ya ini kutokana na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi.

Mbali na faida hizo, pia kutokana na kuwa na sukari yake ya asili huweza kumsaidia mtu katika kupunguza uchovu wa mwili na kutibu maumivu yasiyokuwa na sababu za moja kwa moja.

Sambamba na hayo, juisi ya zabibu husaidia utumbo kufanya kazi kwa ufasaha na kuzuia ukavu wa haja kubwa, lakini pia divai huimarisha afya ya mishipa ya damu katika mfumo wa kumeng’enya, kusaga na kusharabu chakula na viini lishe.

Pia kutokana na madini yaliyomo ndani ya zabibu huifanya divai kuwa ni dawa nzuri inayopunguza maumivu ya tumbo yanayotokana na kujiminya kwa misuli ya kuta za matumbo (antispasmodic effect).

Hizo ndio baadhi ya faida za zabibu ambazo mtumiaji huweza kuzipata pale anapotumia tunda hili mara kwa mara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles