22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Bila Cholestro huwezi kuwa na uhai – 3

vyakula vya wanga
vyakula vya wanga

Na DK. BOAZ MKUMBO,

Unaweza ukajifunza zaidi jinsi gani watu walioharibikiwa na ini ingawa hawanywi pombe. Hivyo usije ukashangaa unapiga picha ya tumbo unaambiwa una dalili za mafuta kurundikana kwenye ini ukashangaa wakati wewe ni mlevi wa sukari na wanga.

NINI KIFANYIKE?

Ancel Keys alipomaliza utafiti wake uliyofanyika kwa miaka 30 alihitimisha kutuambia mafuta ni mabaya. Ukweli wa nadharia hii umebaki changamoto kwani hakuna sehemu yoyote inayoonesha mafuta kutoka kwenye vyakula hubadilishwa kuwa cholestro.

Hakuna sehemu yoyote ambayo inaonesha njia ya kisayansi kwamba mafuta ambayo hayagandi kubadilishwa kuwa cholestro lakini kilichofanyika ni kuhusianisha mambo na kuyafanya yawe ya ukweli.

Profesa Tim Noakes aliwahi kusema “We are chronically ill because of science of Association”.

Inashangaza unahimizwa kula vyakula vya wanga hadi asilimia 60 kwa siku na vijiko 12 vya sukari na kupunguza vyakula vya mafuta.

Kwa nini unahimizwa vyakula ambavyo sote tunajua vinanenepesha? Wewe hilo hutambui?

Simaanishi uache wanga, namaanisha punguza wanga iwe kunyume chake tuishi kama babu zetu kabla ya mapinduzi ya viwanda na kilimo.

Kula wanga asilimia 20-30 na asilimia 60-70, kula vyakula vya mafuta asilia kama babu zetu walivyofurahia chakula chao kikuu kupitia uwindaji, uvuvi na ukusanyaji wa matunda pori.

Sijawahi kusoma mafuta yatokanayo na lishe huhifadhiwa kama mafuta mwilini, jamii imepotoka.

Kwa kuhitimisha cholestro ni rafiki yetu mpendwa na ukiambiwa cholestro ipo juu uliza aina gani iliyopo katika kiwango kikubwa?

Mtu akikuambia “Cholestro is high”

Mambo ya kujiuliza:
-Total cholestro ni ngapi?
-HDL ngapi?
-LDL ni ngapi?
Kisha unaweza kumuuliza pia kama TGA nayo ni ngapi?

Kipimo hicho huitwa Cholestro profile test. Kama hujui hesabu hata hizo ndogo utauguzwa kwa kuwaongezea watu kipato kila upimapo.

Total cholestro (TC) = HDL+LDL

Maana yake ukipata jumla ya cholestro zako 240 halafu LDL ni 90

Hivyo HDL itakuwa 150

Rudi hapo juu
TC=HDL+LDL
HDL =TC-LDL
HDL=240-90

HDL =150

Kinachopima uhatari wa magonjwa ya moyo ni HDL, LDL na TGA. Ndio maana katika mfano wangu hapo juu cholestro zako zipo juu ya 200 lakini kumbe nyingi ni HDL ambazo zinakulinda na magonjwa ya moyo. Kuna sababu ya kushusha cholestro zako?

Kuna mwingine anaweza kukutana na wewe umepima kama hivi:

TGA – high
LDL – high
HDL – low

Total cholestro zipo slightly high

Na unaweza kujiuliza ufanyaje uweze kupunguza tatizo lako kwa kutumia lishe.

Jibu ambalo limekuwa likinishangaza na sintofahamu ya washauri wengi watakuambia “Punguza mafuta kabisa ikibidi usitumie na hakikisha unatumia dona”.

Itaendelea wiki ijayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles