25.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yatamba kutumbua majipu

image17NA ADAM MKWEPU

UONGOZI wa Yanga umetamba kuendelea kutumbua majipu katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuhakikisha wanashinda michezo yake mbalimbali ya ligi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,  Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro, alisema kuwa  wamejiandaa kupata ushindi dhidi ya Stand United katika mchezo wao utakaochezwa leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, licha ya ‘figisufigisu’ wanazoendelea kufanyiwa na  wapinzani wao.

“Tutaendelea kutumbua majipu, licha ya wapinzani wetu kutufanyia figisufigisu, lakini tunawaambia watasubiri sana mwaka huu na hawataweza,” alisema.

Alitoa wito kwa mashabiki wa timu hiyo kwenda kwa wingi kuishangilia uwanjani katika mchezo wao na Stand.

Akizungumza juu ya usajili wao, Muro alisema wamesajili wachezaji wawili, akiwamo aliyekuwa mshambuliaji wa Mbeya City na baadaye Mwadui ya Shinyanga, Paul Nonga na Mniger, Issoufou Boubacar.

Yanga kwa sasa ipo nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 27 mbele ya klabu ya Azam, walio na pointi 26.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles