21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

YANGA YAPOKEA BARUA YA MKWASA KUJIUZULU

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM         |     


UONGOZI wa Yanga umekiri kupokea barua ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa.

Taarifa za kujiuzulu Mkwasa zilienea juzi ikiwa ni muda mfupi kabla ya timu hiyo kucheza na Gor Mahia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika uliochezwa nchini Kenya.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Dismas Ten, alisema ni kweli katibu ameamua kujiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya.

“Katibu alikabidhi barua ya kujiuzulu jana kwa uongozi wa klabu kwa sababu ya kuhitaji kupumzika kutokana na kutokuwa sawa kiafya,” alisema.

Alisema hata hivyo hadi sasa hakuna hatua nyingine iliyochukuliwa baada ya katibu kufanya maamuzi hayo.

Akizungumzia kuhusu kibali cha kocha wao, Mwinyi Zahera, alisema bado wanashughulikia na hata hivyo walianza kwa muda mrefu ila bado hawajapata.

Yanga juzi waliendelea kuburuza mkia katika kundi kundi D, baada ya kufungwa mabao 4-0 na Gor Mahia.

Kwa matokeo hayo, Yanga imebakiwa na pointi moja kutokana na mechi tatu, huku USM Alger iliyoichapa Rayon Sports mabao 2-0 katika mchezo mwingine wa michuano hiyo uliochezwa juzi nchini Rwanda, ikiongoza kundi hilo na pointi saba.

Gor Mahia baada ya ushindi wa juzi, ilijikusanyia pointi tano ikiwa nyuma ya USM Alger, wakati Rayon Sports ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles