24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

KATWILA KUREJESHA MAKALI YA LUIZIO

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM         |      


KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila, amesema anaamini mshambuliaji mpya, Juma Luizio, atakuwa na uwezo kama awali na kuisaidia timu hiyo katika michuano ya kimataifa.

Mtibwa Sugar juzi walitangaza kumsajili Luizio kwa mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Timu hiyo itashiriki michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, baada ya kutwaa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) kwa kuifunga Singida United mabao 3-2, katika fainali iliyochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha mwezi uliopita.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katwila alisema licha ya mchezaji huyo kutoonyesha uwezo mzuri katika timu yake ya Simba, lakini wao bado wanaamini ana uwezo mzuri na ndio maana wamemsajili.

“Tumemsajili Luizio kwa sababu tunaamini bado ana uwezo mzuri na ataisadia timu yetu katika msimu huu na michuano ya kimataifa, kwani licha ya kuwa hajaonyesha kiwango kizuri Simba, awali alipokuwa akicheza hapa alikuwa ni mchezaji mzuri,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,859FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles