24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

Yanga SC, JKU zaikwepa Everton ya England

Na Lulu Ringo

KIKOSI cha Yanga ya Tanzania Bara na kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ya Zanzibar vimeonekana kuikwepa timu ya Everton baada ya kutandikwa mabao matatu kila mmoja katika michezo yake ya jana iliyopigwa Nakuru nchini Kenya kwenye mashindano ya kusaka bingwa wa kombe la SportPesa.

Yanga ilianza kuyaaga mashindano hayo mapema jana na kufuta matumaini ya safari ya Uingereza ambapo wangecheza na Everton inayoshiriki ligi kuu ya England baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Kakamega Homeboyz ya Kenya katika mchezo wa kwanza.

Baada ya kufungwa huko mmoja wa viongozi wa timu hiyo ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji, Salum Mkemi ambaye alitangaza kujiuzulu nafasi yake.

Pia timu ya JKU nayo iliyotupa karata yake ya kwanza jana ilijikuta ikiaga mashindano hayo na kupoteza mwelekeo wa safari ya kwenda Uingereza kucheza na Everton baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Gor Mahia nayo ya Kenya.

Matumaini ya wawakilishi wa Tanzania kushinda taji hilo na kuiwakilisha nchi pamoja na kwenda kucheza mechi na Everton ya England yamebaki kwa Singida United ya Singida na Simba SC ya Dar es Salaam ambayo leo inatupa karata yake ya kwanza kwa kupambana na Kariobang Sharks ya Kenya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,853FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles