26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

SIMBA YAIBANJUA KARIOBANGI YASONGA MBELE

Na LULU RINGO


 

MABINGWA wa Ligu Kuu Tanzania bara Simba Sc wameendeleza ubabe wao nchini Kenya baada ya kuichapa Kariobangi Sharks ya nchini Kenya kwa penati 3-2 kwenye michuanao ya Sportpesa Super Cup inayoendelea nchini humo.

Kariobangi ndio waliokuwa wa kwaza kupiga penati lakini bahati haikua yao kwani walianza kwa kukosa.

Wachezaji wa Simba walioshinda penati zao ni Haruna Niyonzima, Mkude na Erasto Nyoni huku wachezaji Mohamed Husein na Bukaba.

Kariobangi Sharks walikuwa wazuri zaidi ya Simba hasa safu ya kiungo. Kipindi cha kwanza Simba walianza kwa kasi lakini baada ya dakika 10 za mchezo Kariobangi walibadilisha mchezo na kuongeza mashambulizi.

Bahati haikuwa yao kwani safu yao ya ushambuliaji haikujipanga sawasawa licha ya mashambulizi yaliyokua wakiyafanya. Hadi dakika 90 za mchezo kila timu haikuweza kuona lango la mwenzake.

Kwa matokeo hayo Kariobangi Sharks wameyaaga mashindano hayo rasmi wakiungana na Yanga, JKU zote kutoka Tanzania zilizotolewa jana.

Ushindi huo umewapeleka Simba katika hatua inayofuata ya michuano hiyo ambapo itakipiga na Kakamega Homeboys iliotangulia hatua hiyo mapema hapo jana kwa kuifunga Yanga magoli 3-1.

Mashindano hayo yataendelea kesho kwa kuzikutanisha FC Leopard na Singida United.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles