23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga kumng’oa Kihimbwa dirisha dogo

Zainab Iddy, Dar es salaam

BAADA ya kushindwa kuinasa saini ya kiungo mshambuliji wa Mtibwa Sugar, Salum Kihimbwa, dirisha la usajili lililofungwa jana, mabosi wa Yanga wamepanga kumpa mkataba mkali huyo kipindi cha dirisha dogo.

Taarifa ambazo MTANZANIA limezipata kutoka ndani ya Yanga, zinasema kuwa sababu kubwa ya Kihimbwa kutovaa uzi wa njano na kijani msimu ujoa, ni dau kubwa lililotakiwa na Mtibwa Sugar.

“Tumeona bora tusubiri dirisha dogo, labda dau litapungua, lakini kama atakuwa kwenye kiwango kile kile bora, hivi sasa tumeshindwa kwa sababu Mtibwa wamehitaji fedha nyingi sana.

“Mchezaji alikuwa tayari kuja kucheza kwetu, lakini Mtibwa Sugar ndio waliotukwamisha, hivyo tumeona bora tuachane nae hivi sasa,” alisema mtoa habari wetu ndani ya Yanga.

BINGWA lilimtafuta Kihimbwa kuzungumzia hilo ambapo alisema mkataba wa miaka miwili aliosalia nao, ndio uliomzuia kuondoka Mtibwa Sugar.

“Nilisaini mkataba wa miaka mitatu msimu uliopita, nimetumikia mmoja na kubaki miwili, hivyo siwezi kwenda kucheza kwingine kama Mtibwa hawajaruhusu,” alisema.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Mtibwa Sugar, Abubakar Swabur, alisema: “Hatuwezi kumruhusu aondoke wakati ana mkataba na sisi na timu inayomuhitaji imeshindwa, haijawa tayari kutimiza tuliyohitaji.”

Wanajangwani walitaka kumsajili Kihimbwa ili kuiongezea nguvu safu yao ya kiungo tayari kwa michuano ya kimataifa na Ligi Kuu Tanzanai Bara, msimu unaoanza Agosti 23, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles