Harmonize, Mavoko mambo poa

0
1796

Glory Mlay

MSANII kutoka WCB, Rajab Abdul ‘Harmonize’, amesema hana tatizo na staa wa Bongo Fleva Rich Mavoko kama ambavyo watu wanavyodai kwenye mitandao ya kijamii.

Bosi huyo wa Konde Gang, ameliambia MTANZANIA jana kuwa Mavoko ambaye alijitoa WCB ni miongoni mwa wasanii waliomvutia kufanya muziki lakini pia ni mbia wa kazi zake kutokana na wimbo Show Me uliofanya vizuri mwaka juzi.

“Mavoko ni msanii mwenzangu na mbia wangu wa kazi  zangu zaidi ya miaka miwili au mitatu sasa, hivyo lazima nitambue umuhimu wake  na nitaendelea kumpa heshima,” alisema Harmonize ambaye ni miongoni mwa wasanii Afrika watakao tumbuiza katika tamasha la One Africa, New York, Marekani Agosti 10 mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here