28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Yaliyojiri Baada ya Man City Kuthibiti Kombe la UEFA

Mnamo June 10, 2023, uwanja wa Ataturk huko Uturuki ulijawa na shangwe, hapo mashabiki wa Man City wakifurahia ushindi wa timu yao dhidi ya wapinzani wao wenye sifa, Inter-Milan.

Mara nyingi mashabiki kama hawa huwa wanaelewa manufaa yanayotokana na matumizi ya Gal Sport promo code, ambayo hayapungui hata kama ushindi ni 1 – 0 kama ule wa Man City.

Kuzifahamu Timu za Man City na Inter-Milan          

Timu ya Man City, ambayo jina lake kamili ni Manchester City Football Club, ni timu maarufu ya soka kutoka Uingereza, na mji wake ni Manchester. Mji huu pia uko na timu nyingine maarufu ya soka, Manchester United, ambayo jina lake la utani ni ‘the Red Devils’.

Hii timu ya Man City iliundwa mwaka wa 1880 na washiriki wa kanisa la St. Mark’s lililoko mjini Manchester, ingawaje wakati huo wachezaji hawakuwa wameshirikishwa kwa muundo wa klabu maalum. Klabu ilikuja kuundwa kirasmi hapo mwaka wa 1887 ikaitwa  Ardwick Association Football Club. Ilibadilishwa jina ikawa Manchester City Football Club hapo mwaka wa 1894.

Timu ya Inter-Milan, ambayo jina lake kamili ni Football Club Internazionale Milano, inaheshimika sana, sio tu nchini Italy lakini pia duniani. Mji wa timu hii ni Milan, ambako kuna pia timu maarufu ya A.C. Milan.

Michuano ya mwaka huu wa 2023 ya UEFA iliipa nafasi timu ya Inter-Milan kushiriki fainali za UEFA, kwani ni mara ya kwanza timu hii kufaulu hadi fainali yake.

Jambo moja la muhimu ambalo mashabiki wengi wa soka huenda hawajui, ni kwamba ingawapo Inter-Milan iliundwa miaka mingi iliyopita, asili yake ilikuwa mkusanyiko ya wachezaji waasi wa A.C. Milan, ambao hawakuridhika na sharti la kutokubalia klabu hicho kushirikisha wachezaji wa kutoka nchi zingine. Hapo basi, Inter iliundwa mwaka wa 1908 na ikashinda ligi ya Italy mara yake ya kwanza mnamo mwaka wa 1910, chini ya uongozi wa nahodha wake wa kwanza, ambaye alikuwa Mswisi kwa jina Hernst Marktl.

Wale Waliotunukiwa Medali Msimu Huu

Pamoja na kushinda kombe la UEFA hapo Ataturk, Uturuki, wachezaji wa timu ya Man City waliweza kutunukiwa medali ya ushindi kila mmoja, pamoja na meneja wao, Pep Guardiola, aliye na umri wa miaka 52.

Hapo awali, hawa wote walikuwa wametunukiwa medali baada ya kushinda kombe zingine mbili – la Premier league na lile la FA.

Siku chache baada ya ushindi wa UEFA, Pep Guardiola ametambuliwa kibinafsi na Bodi ya Utalii ya Misri, ambayo imemtunuku kombe la kipekee wanaloliita ‘Pharoah trophy’. Meneja huyu wa Man City ambaye ni Mhispania aliipokea zawadi hii akiwa kwenye likizo na familia yake huko Misri, Afrika. Miongoni mwa maeneo aliyoyatembelea pamoja na mke wake, Cristina Serra, na watoto wao watatu, ni mji mkuu wa Misri, Cairo, na eneo la Luxor. Waliweza kujionea vitu kadha vyenye sifa ya kihistoria, miongoni mwao ikiwa ni piramidi kubwa ya Giza na ile sanamu ya kale mno nchini, ya Sphinx.

Inasemekena ya kwamba huenda Pep Guardiola akahama klabu ya Manchester City mwaka wa 2025, hapo mkataba wake ukifika tamati mnamo msimu wa joto. Kama kadirio hili litatimia, Guardiola atakuwa ameiongoza timu hii ya Uingereza kwa miaka tisa mfululizo, hapo mazoezi yao mengi yakiwa yamefanyiwa kwa uwanja wao wa nyumbani wa Etihad.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles