28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

WRM kusherehekea miaka 17 ya huduma Jumatatu ya Pasaka

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Kanisa la The Word of Reconciliation Ministries (WRM), linaadhimisha miaka 17 ya huduma tangu kuanzishwa kwake, huku likijivunia ushiriki wake katika kusaidia maendeleo ya kijamii.

Kilele cha maadhimisho hayo kinatarajiwa kufanyika Aprili 1, 2024 katika kanisa hilo, Kivule-Matembele ya Pili, jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 27,2024, jijini Dar es Salaam, kuelekea kilele cha maadhimisho hayo, kiongozi wa kanisa hilo Nabii Nicolaus Suguye, amesema wamekuwa karibu na jamii kwa kutoa misaada mbalimbali ikiwamo kwa wajane na watoto yatima.

Ametaja misaada mingine kuwa ni kushiriki katika kuvuta umeme na kusapoti ujenzi wa ukuta wa shule ya Kivule na kutoa vifaa tiba kwenye hospitali ya Kivule.

“Tumekuwa karibu sana na jamii kwa kurudisha kwao kile tunachopata. Katika tukio hili la maadhimisho haya, Rais Dk Samia Suluhu Hassan kushiriki na sisi lakini ametuma mwakilishi ambaye ni Waziri wa Ardhi Jerry Silaa,” ameeleza Nabii Suguye.

Kuhusu changamoto kanisa hilo ilizopitia katika kipindi chote cha miaka 17, Nabii huyo amesema hazijawarudisha nyuma wala kuyumba bali zimewajenga zaidi kiimani.

“Hakuna huduma yoyote inakosa changamoto na kukataliwa. Nimepitia kubezwa na kukataliwa na tulifungiwa miezi mitatu lakini changamoto zote hizo zimenikomaza,” amesema.

Amefafanua kuwa pamoja na huduma za maombezi zitakazokuwepo siku hiyo, pia zitakuwepo burudani kutoka kwa waimbaji wa nyimbo za injili na wachekeshaji wanaoigiza sauti za viongozi mbalimbali.

“Pia kutakuwepo na chakula cha kila aina, ambacho kitakuwa ni bure kwa kila atakayehudhuria na usafiri wa bure utaanzia maeneo ya Banana,” amesema Nabii..

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles