24.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Elimu, Digital Pipeline ya UK wazindua mradi wa elimu kwa njia ya mtandao

SARAH MOSSI, DAR ES SALAAM

KATIKA kuungana na juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, Shirika la Digital Pipeline UK, kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia wameanzisha mradi mkubwa utakaobadilisha na kuboresha utoaji wa elimu nchini kuanzia shule za msingi za serikali hadi kidato cha sita kwa njia ya mtandao salama (Secured School Network) utakaobeba mtaala (curriculum) na vitabu vya maarifa mbalimbali vinavyokwenda na wakati.

Mtaala huo  utawafanya walimu na wanafunzi kujinoa ipasavyo na kuwa wabunifu wanaoweza kushindana katika ulimwengu wa maarifa kwa wakati. (Communication Tool).

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Digital Pipeline Uk, Abraham Sangiwa alisema mradu huo unafadhiliwa na Bill and Melinda Gate Foundation, Metropolitan Police UK, National Health Services UK na  Vauxhall Motors UK.

Hafla ya uzinduzi wa mradi huo kabambe ilifanyika katika ofisi kuu Priory Park jijini Kent nchini Uingereza

Uzinduzi huo pia ulishuhudiwa na wadau mabalimbali akiwamo Deputy Lieutenant of Kent Trevor Sturgess, Bevil Williams C.E.O at Digital Pipeline, board members, wafanyakazi wa Digital Pipeline UK na wadau mbalimbali

Sangiwa aliishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kuahidi kuendelea kuwa Balozi wa nia njema katika mradi huo  wa Digital Campus na huku akisisitiza haikuwa kazi rahisi kufanikisha mradi huo kwa Tanzania.

Digital Pipeline UK inafanya shughuli zake katika nchi zaidi ya 27 barani Afrika, nchi nane Bara la Asia, baadhi ya nchi Bara la  Ulaya, Amerika ya Kati na Kusini.

Sangiwa alisema mradi huo ulipendwa na kila nchi kwani unajenga  Digital Campus Plant kubwa na ya pekee barani Afrika.

“Lakini kutokana na uzalendo na uelewa kwa timu nzima ya Wizara ya Elimu na viongozi wake na  kwa kuzingatia vigezo vilivyo wazi kwa Serikali ya Tanzania vimesaidia kuleta mradi huu wenye manufaa makubwa nchini.

“Tumeingia makubaliano na Wizara ya Elimu kufanya mradi huu kwa kusaini  MoU ambapo leo hii sehemu ya kwanza kuhudumia zaidi ya shule elfu moja unaanza kwa kupakia makontena haya ya vifaa husika na kuondoka hapa Uingereza kuelekea Tanzania, kwani serikali ya Tanzania kupitia Tanzania Institute of Education imekwishatoa eneo lilipo Mikocheni jijini Dar es Salaam  ambapo kutajengwa Digital Campus kubwa itakayokuwa ikipokea vifaa vya mradi, pia mahali hapa patakuwa kituo kikubwa cha “recycling and assembling Plant” kwa ajili ya e learning na kufanya mageuzi kwa kutumia portal mbalimbali za “smart learning” mtandaoni.

“Digital Campus itatoa ajira, mafunzo na huduma  kwa Watanzania wa kawaida, wafanyabiashara, serikali na mashirika mbalimbali yatakayotaka kuphase out thier ICT equipment safely with certification of data wiping under EU LAWS (World Standard) and US Military Standards,” alisema Sangiwa

Kwa mujibu wa Sangiwa wanatarajia mradi huo utaanza na shule elfu moja na kuleta computers, laptops, printers na projectors zaidi ya arobaini elfu kwa awamu ya kwanza.

“Tunaamini kutoa vifaa hivi pekee bila kufanikisha upatikanaji wa mtandao hasa kwa maeneo ya vijijini itakuwa vigumu, hivyo Digital Pipeline kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi kupitia kampuni ya TTCL itaanda mkakati wa kufanikisha upatikanaji wa mtandao  vijijini.

“Digital Pipeline kwa kushirikiana na “Avanti iknowledge program” wataunganisha mtandao kwa njia ya satellite, pia kusaidia upatikanaji  wa umeme kwa njia ya “solar power” supply of panels and fittings ili kuweza kufanikisha malengo ya mradi huu muhimu katika kuboresha utoaji wa elimu.

Sangiwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio UK (TZUK Diaspora) alisema kutakuwa na mafunzo kwa walimu namna ya kutumia smart e learning equipments  na kutoa vitabu na majarida ya elimu yanayokwenda na wakati.

Rais Dk. John  Magufuli na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na timu yake katika Wizara wamejitahidi sana kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bure kwa kujenga madarasa na shule nyingi, sisi Watanzania tunaoishi hapa UK na sehemu nyingine ulimwenguni tunahitaji kusaidia katika ubora wa elimu ili lengo la Tanzania ya Viwanda liweze kutimia kwa kutumia vipaji na ubunifu toka ndani ya nchi ambao unapotea kwa kiasi kikubwa hasa maeneo ya vijijini kutokana na kukosa walimu wenye kuweza kujiongezea maarifa kwa njia ya mtandao wa elimu duniani unaokwenda na wakati, pia wanafunzi kukosa vitabu vya sasa (up to date texts book) ambavyo ni rahisi kuvipata chini ya smart secured learning program.

“Tanzania ni nchi inayokua kwa kasi kiuchumi na idadi ya watu, hivYo basi mahitaji ya elimu yanazidi kuongezeka na Digital Education itasaidia kukwamua kizazi kijacho, tunafahamu baadhi ya concern kuhusu usalama na matumizi mabaya ya mtandao, lakini jambo hili litadhibitiwa na Avanti iknowledge na wadau wengine tulionao katika utoaji elimu kwa njia ya mtandao ambapo hudhibitiwa kwa mtumiaji,” alisisitiza Sangiwa.

Uzinduzi wa mradi ho unatarajiwa kufanyika rasmi hivi karibuni mara baada ya makontena yenye vifaa vya mradi kuwasili katika Bandari ya Dar es Salaam,  chini ya usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Digital Pipeline UK

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles