24.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Serikali yahaha kutafuta soko la tumbaku

WALTER  MGULUCHUMA-KATAVI

 SERIKALI imeanza kutafuta masoko mapya ya zao la tumbaku baada ya kampuni ya ununuzi yaliyopo sasa  kupunguza idadi ya kilo kila mwaka kwenye vyama vya msingi vya ushirika.

Kauli  hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya  Kilimo, Mathew Mtigumwe wakati alipokuwa  akizungumza na wadau mbalimbali wa kilimo mkoani Katavi.

 Alisema kutokana na kampuni hizo kushusha idadi ya kilo za tumbaku walizokuwa wakinunua kwa wakulima kupitia kwenye vyama vyao vya ushirika vya msingi  Serikali imeona itafute masoko mapya ya  zao la tumbaku kukabiliana na tatizo hilo.

Katibu mkuu huyo alieleza kuwa wameiagiza Bodi ya tumbaku nchini kwenda kwenye nchi zinatumia zaidi tumbaku kutafuta soko la zao hilo.

 “Mpaka  sasa   kuna kampuni moja ambayo tayari imeonyesha nia ya kununua tumbaku na tunatarajia kuanza kununua kilo milioni moja msimu huu, hivyo jitihada za kutafuta masoko mengine mapya zinaendelea kufanywa na  Serikali.

Awali baadhi ya  wadau wa tumbaku Mkoa wa Katavi walionyesha wasiwasi wao kuhusu soko la zao hilo kutokana na kushuka kwa ununuzi wa kutoka kilo milioni 16 miaka mitatu iliyopita hadi kufikia kilo milioni sita kwa msimu huu wa kilimo.

Mmoja wa wadau hao, Selemani Kaitila alisema ununuzi wa tumbaku imekuwa ukishuka mwaka hadi mwaka kutokana na kampuni zinazonunua tumbaku huku mapato ya halmashauri yakizidi kuporomoka kwa kukosa ushuru unaotokana na zao hilo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,400FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles