28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Win Princess yamrejesha Gigy Money Bongo

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

MSANII wa muziki wa Bongo fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’, ambaye pia ni Balozi wa kampuni ya michezo ya kubahatisha, Win Princess amefunguka jinsi kampuni hiyo ilivyomsaidia kurudia Tanzania baada ya kukwama nchini Uingereza alipokuwa akifanya shoo licha ya yeye kuwa Balozi wa Kampuni hiyo.

Gigy Money ameyasema hayo juzi katika uzinduzi wa namba mpya ya kituo cha msaada wa michezo ya kubashiri ya kampuni ya Win Princess iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

“Nimekuwa nikijisikia fahari na kujivunia kuwa Balozi wa kampuni mbalimbali lakini kwa Kampuni ya kubeti ya “Win Princess” nimekuwa nikicheza michezo ya kubahatisha kupata Sh 400,000 fedha hiyo nikaenda kulipa ada ya mtoto wangu.

“Pamoja na kampuni hiyo kunipatia tiketi ya kurudi nchini baada ya kukwama nchini Uingereza wakati wa shoo yangu kusitishwa,” amesema Gigy Money.

Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hakan Aric, amesema huduma hiyo waliyozindua wateja watapiga simu bure kwa lengo la kupata msaada.

“Kutokana na mchezo huu wa kubahatisha kushika kasi na wateja wengi kuongeza katika kampuni ya Win Princess hivyo tumetangaza rasmi namba itakayowawezesha wateja wetu kufikiwa kwa urahisi katika kupata huduma za kubashiri,” amesema Aric.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles