MKURUGENZI wa shindano la X Factor, Simon Cowell, juzi alijikuta akidondosha chozi kutokana na wimbo ulioimbwa na mmoja wa washiriki katika shindano hilo, Josh Daniels.
Wimbo huo aliuimba kwa hisia kubwa akielezea kifo cha rafiki yake wa karibu aliyepoteza maisha yake huku akiwa na umri wa miaka 18.
Julai 5 mwaka huu, mkurugenzi huyo alimpoteza mama yake kipenzi, Julie Brett, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 89, kutokana na kumbukumbu ya kifo cha mama yake, Cowell alijikuta akidondosha chozi bila kutarajia.
Kipande cha mistari hiyo kinasema: ‘Nimempoteza rafiki yangu kipenzi miaka miwili iliyopita ndiyo maana baadhi ya mambo yangu yanayumba.”