24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Kotto: Msiwachague kwa uzuri wa filamu na nyimbo zao

NA FARAJA MASINDE

MMILIKI wa bendi ya muziki wa dansi ya Kotto, Said Mohamed, amewataka Watanzania wawapime kwa sera zao wasanii wote wanaogombea nafasi mbalimbali za uongozi badala ya kuangalia majina yao tu.

Kotto alisema wapo wasani wengi waliokimbilia siasa lakini hawana na wala hawajui sera zao ni nini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, hivyo wananchi wanatakiwa kuwapima ndipo wawachague kwa ajili ya maendeleo yao ya miaka mitano ijayo.

“Uchaguzi huu umejumuisha wasanii wa kila aina, waigizaji tusiwape kura kutokana na umahiri wao katika uigizaji bali kwa sera zao na waimbaji pia tusiwape kura kutokana na ubora wa nyimbo zao bali tuwape kura kutokana na sera zao zitakazotufikisha miaka mitano kwa usalama na maendeleo bora,” alisema Kotto.

Msanii huyo aliyewahi kuwika na wimbo wa ‘Mombasa’ na ‘Maisha ya Mjini’ aliyowashirikisha Chegge na Fid Q, anatarajia kuachia wimbo wake mpya aliouita ‘Niwewe tu’ aliomshirikisha Diamond Platnumz.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles