25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wiki ya Asasi za Kiraia kuanza Oktoba 23, mwaka huu jijini Dodoma

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

WIKI ya Asasi za kiraia (AZAKI) inatarajiwa kuanza Oktoba 23 hadi 29 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambapo jumla ya asasi za kiraia 1,500 zinatarajiwa kushiriki.

Wiki hiyo itatumika kujenga mahusiano mazuri baina ya Serikali na asasi za kiraia, mijadala na majadiliano pamoja na utoaji wa tuzo kwa Taasisi ambazo zinamchango mkubwa kwa serikali.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Agosti 12, mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society, Francis Kiwanga amesema lengo la wiki hiyo ni kutambua umuhimu wa asasi za kirai katika ufanyaji kazi wao kwa kushirikiana na wananchi pamoja na serikali.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Hakirasilimali, Racheal Chaganja ametaja malengo mengine kuwa ni kuimarisha na kujenga mahusiano mazuri baina ya serikali, watu binafsi pamoja na Asasi za kiraia katika ujenzi wa taifa.

“Katika wiki hiyo kutakuwepo na mijadala na midahalo mbalimbali pamoja na maonyesho ya kazi zinzofanywa na Asasi za kiraia kama msaada wa masuala ya kisheria,”amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CBM, Nesia Mahenge amesema wiki hiyo itaenda sambamba na utoaji wa tuzo kwa mashirika na taasisi ambazo zimekuwa na mchango mkubwa kwa serikali na tuzo kwa vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikitoa taarifa kuhusiana na kazi za Asasi za kiraia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles