28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Chama aungana na Kisinda RS Berkane

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Kiungo wa Simba, Clatous Chama amejiunga na timu ya RS Berkane ya nchini Morocco ambayo amekwenda nyota wa Yanga Tuisila Kisinda.

Licha ya kwamba Simba haijatoa taarifa kamili ya mchezaji huyo, kuondoka, wachezaji hao wameonekana wakifanya mazoezi na kikosi hicho kinachonolewa na kocha raia wa DR Congo, Florent Ibenge.

Mchezaji mwingine anayeondoka Simba ni  Luis Miquissone anakwenda Al Ahly ya nchini Misri, huku Chriss  Mugalu naye akihusishwa kujiunga na Far Rabat.

Wanamsimbazi hao  wapo nchini Morocco kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles