27.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

WHITEDENT KINARA SUPER BRAND 2017

NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM 


DAWA ya meno ya Whitedent imepata tuzo ya  kimataifa ya ubora inayojulikana kam SuperBrand, huku nafasi ya pili ikishilikiwa na Foma Gold.


Tuzo hiyo imetolewa baada ya utafiti  uliofanywa na Kampuni ya Kimataifa ya utafiti wa ubora wa bidhaa  ya nchini Uingereza inayojulikana kama The Centre for Brand Analysis.


Katika utafiti huo uliofanyika katika  masoko kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza kwa kuwahusisha watumiaji wa bidhaa na huduma zaidi ya 1,000.

Katika utafiti huo pia sabuni maarufu ya unga ya Foma Gold nayo imebainishwa kuwa ni bidhaa bora nchini  na imetunukiwa tuzo ya SuperBrand. 


Akizungumzia matokeo hayo, Ofisa Mtendaji wa Taasisi ya The Centre for Brand Analysis, Stephen Cheliotis, alisema: “Inafurahisha kuona chapa nyingi za Tanzania zinaendelea kushikilia rekodi ya ubora na kuendelea kupata tuzo za SuperBrand mwaka hadi mwaka.
 
“Mwaka huu chapa nyingi zimeweza kuendelea kushikilia rekodi ya kuingia kwenye  chapa bora 20 zinazoongozwa kwenye masoko na mwaka huu chapa za bidhaa kwenye kundi la  usafi na afya za Whitedent na Foma Gold zimefanya vizuri na zinakubaliwa na wengi kwenye masoko.” 


Ofisa Mtendaji huyo alisema matokeo hayo yalizingatia maoni ya wataalamu wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ukihusisha pia makampuni ya hapa nchini yanayotumia nembo na chapa za biashara za kimataifa kama vile TOYOTA na Pepsi ambapo chapa 10 zimeingia kwenye chapa 20 bora.


Aisha alisema  utafiti huo ulifanyika katika mgawanyo wa makundi ya taasisi za  fedha, vyakula na vinywaji, magari na utoaji wa huduma kwa jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles