27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Wenger atangaza kurudi uwanjani

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa zamani wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, amefunguka kwa mara ya kwanza na kusema kuwa, anatarajia kurudi uwanjani mwanzoni mwa msimu wa 2019.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 69, amekuwa nje ya uwanja tangu alipoachana na Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita, baada ya kuwa ndani ya klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 22.

Hata hivyo, kocha huyo ameweka wazi kuwa, ataonekana uwanjani, lakini si katika Ligi Kuu nchini England kama watu wanavyodhani. Alikuwa anahusishwa kutaka kutua katika klabu ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid.

“Ninaamini mwanzoni mwa msimu wa 2019 nitaanza kuonekana viwanjani, kwa sasa nipo kwenye mapumziko mazuri, nimekuwa nikitumia muda mwingi kuangalia soka, lakini nimekuwa nikiongea mara kwa mara kwamba, ujio wangu hautakuwa kwenye Ligi Kuu England, kwa kuwa nimekuwa hapo kwa kipindi kirefu sana.

“Hata hivyo, siwezi kuweka wazi kuwa nitakuwa kwenye timu gani, nitakuwa sehemu fulani lakini sijui ni wapi, muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi,” alisema Wenger.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,406FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles