30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

Wenger aponda uhamisho wa Paul Pogba

FBL-EUR-C1-JUVENTUS-TRAININGLONDON, ENGLAND

KOCHA wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger, ameuponda uhamisho wa kiungo wa klabu ya Juventus, Paul Pogba, kujiunga na mashetani wekundu, Manchester United.

Nyota huyo anatarajia kuvunja rekodi ya usajili duniani atakapofanikiwa kujiunga na klabu ya Manchester United kwa kitita cha pauni milioni 100, ambapo kabla ya usajili huo, mchezaji ambaye anaongoza kwa kusajiliwa kwa kitita kikubwa ni Gareth Bale, ambaye alijiunga na Real Madrid akitokea Tottenham kwa pauni milioni 86.

Kwa sasa usajili ambao unasubiriwa na idadi kubwa ya mashabiki na wadau wa soka duniani ni juu ya kiungo huyo raia wa nchini Ufaransa mwenye umri wa miaka 23.

Kutokana na kiasi hicho cha fedha, Kocha Wenger amekiponda na kudai kwamba ni kikubwa na hakuna sababu ya kutumia fedha zote hizo kwa ajili ya kumsajili mchezaji mmoja.

“Kwa upande wangu nitanunua mchezaji ambaye atakuwa na mchango mkubwa katika kikosi changu, kikubwa ninachokiangalia ni kupata mchezaji mwenye sifa zote, lakini si kununua kama wengine ambavyo wanafanya.

“Hata ukiwauliza mashabiki ni mchezaji gani ambaye anaweza kufaa katika kikosi watakuambia, hivyo siwezi kutumia fedha nyingi kumnunua mchezaji mmoja kama ambavyo wanataka kufanya Manchester United kwa Pogba.

“Timu ambayo inataka kushindana katika kumsajili Pogba ni ujinga, kwa kuwa fedha zinazotakiwa ni nyingi, lakini kama ipo klabu ambayo ina uwezo wa kumsajili basi inaweza kufanya hivyo, lakini kwa upande wangu siwezi kufanya hivyo,” alisema Wenger.

Hata hivyo, mchezaji huyo amedai kwamba soka la sasa ni tofauti na miaka ya nyuma, hivyo kuna uwezekano wa kuzidi kuyaona mengi kwa miaka inayokuja katika biashara ya soka.

“Kama leo hii mchezaji anauzwa pauni milioni 100, basi ninaamini ipo siku tutakuja kusikia thamani ya mchezaji ikifika pauni milioni 200 hadi 300 kutokana na ushindani.

“Hii hali tutakuja kuiona miaka michache ijayo bila kujali uwezo wa mchezaji mwenyewe, ila kwa upande wangu siwezi kusema kama nitaweza kufanya usajili wa fedha kama hizo kwa mchezaji mmoja,” aliongeza.

Arsenal kwa sasa inahangaika kutafuta beki wa kati ambaye atachukua nafasi ya Per Mertesacker, ambaye anadaiwa kuwa majeruhi, klabu hiyo inamuwinda beki wa Valencia, Shkodran Mustafi, mwenye umri wa miaka 24, inadaiwa kwamba thamani ya mchezaji huyo ni pauni milioni 42.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles