23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Milner ataka kuachana na timu ya taifa

Milner-City-549002LONDON, ENGLAND

KIUNGO wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya England, James Milner, amepanga kukutana na kocha wa timu hiyo ya taifa kwa ajili ya kumwambia kuwa anataka kuachana na timu hiyo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30, amedai kwamba michuano ya Euro 2016 ilikuwa ya mwisho kwake, hivyo anataka kukutana na kocha mpya wa timu hiyo, Sam Allardyce hivi karibuni.

Mchezaji huyo amedai kuwa anaamua kuchukua maamuzi hayo kutokana na timu hiyo kufanya vibaya katika michuano hiyo ya Euro, huku kikosi cha England ‘Three Lions’ kikiwa na wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa.

“Natarajia kukutana na kocha Sam kwa ajili ya kufanya mazungumzo juu ya maamuzi yangu. Kwa umri wangu kuzunguka na timu bila mafanikio yoyote ina maana?

“Lakini ninaamini kwa upande wa wachezaji vijana ni wakati wao wa kuzunguka na timu na kupata uzoefu kwa ajili ya kutetea taifa.

“Nadhani kwa upande wangu naweza kusema inatosha baada ya kushiriki michuano mikubwa minne nikiwa na timu hiyo, najua kuwa imenipa jina kubwa kwa kipindi chote nilichokitumikia,” alisema Milner.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles