27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Wema Sepetu awafunda wabunifu chipukizi

Wema SepetuMISS Tanzania 2006, ambaye pia ni mwigizaji wa filamu za bongo, Wema Sepetu, amewataka wabunifu chipukizi wa mavazi na mitindo nchini walitumie vizuri jukwaa la mitindo la Lady In Red Fashion Show 2016, ili wafikie malengo waliyojiwekea.

Wema alitoa rai hiyo alipokuwa akizungumza nao kuhusiana na onyesho litakalofanyika Januari 31, katika ukumbi wa Danken House, uliopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

“Kwa sasa mnatakiwa muwe wabunifu zaidi mje na vitu vya kipekee ili kazi hizo ziwe chachu na kivutio kwa wateja wenu, pia iwaongezee mashabiki wa mavazi na ajira yenu, iwe ya uhakika na soko,’’ alieleza Wema.

Naye Mkurugenzi wa Fabak Fashions na muandaaji wa jukwaa hilo, Asia Idarous, alisema jukwaa hilo ni shule na daraja la wabunifu wa mavazi na mitindo, hivyo litaendelea kuenziwa ili lizidi kuzalisha wabunifu wengi zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles