21.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Albamu ya marehemu Bowie yaongoza kwa mauzo

DU0105-ZQQYYY-001NEW YORK, MAREKANI

LICHA ya msanii wa Marekani, David Bowie kufariki dunia, albamu yake ijulikanayo kwa jina la ‘Black Star’ inaongoza kwa mauzo nchini humo.

Albamu hiyo imetolewa siku mbili kabla ya kifo chake, ambapo imeshauza nakala 181,000 na kuipiku albamu ya Adele iliyokuwa ikiongoza kwa mauzo.

Msanii huyo alifariki Januari 10 mwaka huu, baada ya kuugua kwa miezi 18 kutokana na saratani na albamu yake iliwekwa sokoni Januari 8.

Black Star ndiyo albamu ya kwanza nchini Marekani kuuza sana baada ya albamu ya marehemu Michael Jackson, ambaye alitamba na albamu yake ya ‘This is it’, iliyoongoza katika mauzo Novemba mwaka 2009.

Albamu nyingine za Bowie pia ziliorodheshwa miongoni mwa albamu 200 za Billboard wiki hii, huku albamu ya ‘The best of Bowie’ ikishika nafasi ya nne na ‘The Rise and Fall of Ziggy Stardust’ na ‘Spiders from Mars’ zikishikilia nafasi ya 21.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles