24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

WCF YAWAPIGA MSASA MADAKTARI 504

Madaktari  zaidi ya 504 nchini wamepewa mafunzo maalumu ya utambuzi wa magonjwa yatokanayo na kazi yatakayowezesha kutoa tathmini sahihi wakati wa malipo ya fidia kwa wanyakazi.

Kauli hiyo imetolewa mjini hapa kwenye Mkutano Mkuu wa kwanza wa mwaka wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),  uliofunguliwa leo Novemba 29 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama jijini Arusha.

Mhagama ameutaka mfuko huo kuzingatia sheria ili kila anayetakiwa kufidiwa na mfuko huu anufaike na waajiri wazingatie usalama makazini kwani ajali na vifo makazini hupoteza nguvu kazi ya taifa.

Kw aupande wake Naibu Waziri, Anthony Mavunge amesema ofisi yake itaendelea kuwajengea uwezo madaktari nchini katika suala zima la utambuzi wa magonjwa yatokanayo na kazi.

“WCF inaendelea kukua niwaombe waajiri nchini kujisajiri kwani bila kufanya hivyo sheria zitachukua mkondo wake ikiwamo kufikishwa mbele vya vyombo vya sheria. Fidia kwa wafanyakazi ni kinga muhimu,” amesema Mavunde.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Emmanuel Humba  amesema utolewaji wa mafunzo hayo umelenga kuwawezesha madaktari kuwa na uelewa mpana wa namna ya utambuzi kwa watu wanaofidiwa.

“WCF imeundwa kisheria kwa ajili ya kufidia wafanyakazi wanaougua wakiwa kazini, kupata ajali na kupoteza maisha, sasa katika shughuli za aina hii ni lazima madkatari wadau muhimu katika suala hili wawe na mafunzo maalumu. Mafunzo haya tumefanikiwa kuyatoa kwa madaktari 504 kupitia uwezeshwaji wa Shirika la Kazi Duniani (ILO),” amesema Humba.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa WCF,  Masha Mshomba amesema matarajio ya mfuko huo kuwa ni kutoa huduma bora, kujenga uwezo wa taasisi na kuboresha mifumo ya utendaji kazi.

Aidha Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri nchini Agrey Mulimuka aliomba Serikali kuangalia upya suala la uchangia katika mfuko kwani halipo sawa kwa sasa.

“Huu ubaguzi kwenye uchangiaji ntaendelea kuupigia kelele, naomba usiwepo kwanini sekta ya umma waajiri wachangie asilimia 0.5 na sekta binafsi waajiri wachangia asilimia moja? Amehoji Mulimuka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles