23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 9, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI MWENYE UMRI MDOGO AUAWA SOMALIA

MOGADISHU, SOMALIA


WAZIRI  mwenye umri mdogo zaidi nchini Somalia, Abas Abdullahi Sheikh Siraji, ameuawa kwa kupigwa risasi mjini hapa baada ya msafara wake kushambuliwa karibu na Ikulu.

Waziri huyo wa Ujenzi wa Umma alipata umaarufu mkubwa baada ya kushinda kiti cha ubunge kuliwakilisha Jimbo la Jubbaland licha ya ugeni katika siasa.

Sheikh Siraji (31), ambaye alikuwa kipenzi cha wengi nchini hapa aliwahi kuishi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyopo nchi jirani ya Kenya akiwa mtoto na kisha kurejea hapa mwaka jana kushiriki uchaguzi mkuu.

Watu wengi walimtaja kama mtu machachari  miongoni mwa mawaziri na saa chache kabla ya kuuawa kwake alizindua mradi wa ujenzi wa jengo kwa ajili ya watumishi wa umma.

Wizara ya Habari ya Somalia imetoa taarifa ikisema washukiwa wa mauaji hayo tayari wamekamatwa.

Taifa hili la Pembe ya Afrika lililoathirika na machafuko liliendesha uchaguzi wake Februari mwaka huu ambapo Mohamed Abdullahi ‘Farmajo’ alichaguliwa kuwa rais mpya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles