WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA KAMATI YA KULINDA HAKI ZA WASANII

0
681

BRIGHITER MASAKI -DAR ES SALAAM.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amezindua rasmi kamati ya kusimamina na kulinda kazi za wasanii.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mwakyembe amewapongeza mawakili waliopigania haki za wasanii kama marehemu Steven Kanumba pamoja na Mrehemu King Majuto hadi wamepata stahiki zao.

“Msanii yoyote anatakiwa asiingie mkataba wowote pasipo kuwa na mwanasheria wakupitia makubaliano yao wote wawili kwa lugha inayoeleweka.

“Nimemteuwa Sara ndiye Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mwalimu wa Chuo cha Dar es Salaam, Dkt Dora mwanasheria wa Cosota, na Dkt Kilonzo Mkurugenzi wa bodi ya filamu pamoja na Willard Tailo mwakilishi wa Bodi ya filamu”anasema Mwakyembe

Aidha aliongeza kuwa kuna vijana kumi wamefanyishwa kazi na kutokupata malipo yao baada ya kurekodi filamu na baadae kutokulipwa wakawaachwa njia Panda na waliokubaliana nae akawakipia na kwenda nje ya nchi tutalishughulikia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kuwa wanakutana na changamoto nyingi kutokupewa ushirikiano na Makampuni husika wanapo yahitaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here