RC MAKONDA ATENGUA KAULI YA SOPHIA MJEMA

0
1036

BRIGHITER MASAKI – DAR ES SALAAM.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam ametangaza kutengua kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema ya kuwataka wanakazi wa Ilala kumwabudu Mungu siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili bali waabudu watakavyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema Leo, ofisini kwake Makonda anasema kuwa jambo la imani ni la mtu binafsi mtu yoyote hapaswi kuliingilia.

“Naitengua kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa kusema kuwa mtu anapaswa kuabudu muda gani na siku gani, ila muda wowote anapojisikia.

“Upande wa Imani serikali haina dini natengua kauli ya Mkuu wa Wilaya ya IIala Sophia Mjema, tuhamasishe watu wafanyekazi ila tusiingilie imani ya mtu binafsi kwa kuwa ibada haina siku muda wala saa ya kumwabudu Mungu”alisema Makonda

Aidha alisema kuwa atawakamata wakandarasi wote wasiofanyakazi na kukabizi miradi kwa wakati kwa huku wakiwa na visingizio tofauti.

Alisema kuwa kuna wakandarasi WA Mtongombe, Kivule, Buguruni Kisiwani Tabata masoko wamekuwa wakitoa taarifa na nyaraka za uwongo tofauti na utendaji wao nitawakamata.

“Nilisema kuwa mkandarasi yoyote mwenye matatizo na kazi saiti kwake alete malalamiko kwa Mkuu wa mkoa hakuna aliyeweza kuleta malalamiko wakati kazi haziendelei saiti

Aidha aliongeza kuwa atafunga mwaka kivingine akisaidia watoto 100 wenye Matatizo ya Moyo kwa kutangaza kamati itakayo simamia kuwasaidia wenye huitaji.

Kamati itaongozwa na Chalse Kimei ndie Mwenyekiti wa kamati pamoja na wajumbe kutoka kwenye taasisi mbalimbali ili kusaidia watoto 100 kupata matibabu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here