24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu: Uhakiki korosho umejaa rushwa

NA FLORENCE SANAWA, MTWARA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema uhakiki wa korosho kuanzia kilo 1,500 na zaidi umejaa rushwa.

Amezitaka mamlaka husika kukamilisha kazi hiyo ifikapo Februari 5, mwaka huu.

Alikuwa akizungumza wakati wa kikao kilichojumuisha wakuu wa mikoa sita na wilaya zinazolima   korosho mkoani Mtwara jana.

Majaliwa  alisema kuwapo   mazingira ya rushwa katika uhakiki kunachochea ucheleweshaji wa malipo kwa wakulima.

Mikoa hiyo,ni Lindi, Mtwara,Pwani, Ruvuma,Tanga na Ruvuma.

Alisema kazi hiyo  inatakiwa ikamilike Februari 5 na malipo yote yakamilike Februari 15, mwaka huu.

Kwa sababu  hiyo, kazi ya uhakiki aliikabidhi kwa wakuu wa wilaya na kamati za ulinzi na usalama za wilaya kwa kushirikiana na timu za uhakiki.

“Nina taarifa za kuwapo   mazingira ya rushwa kwenye uhakiki, mkulima anatoa rushwa ili apitishiwe kilo zaidi ya 1,500, endapo mtu yeyote akibainika kutoa rushwa asiachwe, ashughulikiwe.

“Kamati zote za ulinzi na usalama jiridhisheni wakati mnasimamia kazi hii  kwa kuwa tunaona idadi ya wenye kilo zaidi ya 1,500   waliolipwa ni ndogo zaidi  ikilinganishwa na wakulima wengine.

“Kwa kweli hatutarajii kusikia bado mnahakiki ikifika muda niliowambia, lazima tusimamie kwa ukamilifu  kuondoa ulanguzi   kuwanufaisha wakulima.

“Wakulima wote wenye akaunti zenye matatizo ama wale ambao hawajachukua fedha zao kwenye akaunti zao, majina yatolewe   wapewe taarifa.

“Wenye matatizo waeleweshe ili warekebisha taarifa kwenye akaunti zao,” alisema Majaliwa.

Alisema vyama vya ushirika ndiyo vyenye dhamana ya kukusanya mazao.

Waziri Mkuu alisema  kuwapo   chama cha ukusanyaji wa mazao   hakitakubaliwa kufanyakazi kwa kuwa ushirika ndiyo pekee unaotakiwa kusimamia.

Alisema   chama cha ushirika wa mazao kilichosajiliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani  hakitatambulika kufanya shughuli za ushirika kwa kuwa wizara hiyo husajiri NGOs tu.

Naye  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara, Yusuph Nannila alisema taarifa za uhakiki ziko juu  lakini wakulima waliolipwa ni wachache.

Alisema kitendo cha kuwacheleweshea wakulima malipo ya korosho kimesababisha baadhi ya huduma kuathirika, ikiwamo elimu na afya.

Aliomba kasi iongezwe   wakulima waweze kulipwa.

“Unajua tufikie wakati tuwe wa kweli, malipo hayaendi kwa kasi inayotakiwa, tusipende kudanganyana katika hili.

“Tuwe wakweli  kuondoa mikanganyiko iliyopo katika malipo ya korosho.

“Katika hili wakulima wanahakikiwa mara nyingi kuliko maelezo.

“Ifike wakati tuelekezane tuwe wa kweli, mmetuchelewesha kwenye malipo yetu,” alisema Nannila. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles