23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI MKUU KUFUNGUA MKUTANO LAPF

Na ASHA BANI


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa tisa wa wadau wa Mfuko wa Pensheni utakaofanyika Machi 9 na 10, jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Meneja Mawasiliano wa LAPF,  James Mlowe, alisema mkutano huo utakaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa AICC, ni maalumu kwa kutoa taarifa za uendeshaji wa mfuko na kuwapa wadau kutoa maoni mbalimbali ili kuboresha utendaji wa mfuko.

Alisema mikutano hiyo hufanyika ili kutekeleza maagizo ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA).

Aliongeza kuwa kaulimbiu ya mkutano huo wa mwaka ni ‘Kuibua fursa endelevu za ajira kwa maendeleo ya Hifadhi ya Jamii ya Taifa’.

“Pamoja na mambo mengine kwenye mkutano huo mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwemo mada inayohusu kaulimbiu, nyingine itahusu utendaji wa mfuko kwa kipindi cha mwaka 2016-2017, taarifa za uwekezaji pamoja na hesabu za mfuko ya mwaka 2015 na 2016,” alisema Mlowe.

Aliongeza kuwa katika siku ya kwanza ya ufunguzi watazindua huduma ya mkopo wa kujikimu ijulikanayo kwa jina la Maisha Popote na LAPF kwa kushirikiana na LAPF.

Alisema kwa kuwa siku ya ufunguzi ni Siku ya Figo Duniani basi LAPF itatumia fursa ya siku hiyo kwa wadau wote kupima figo bure kutoka kwa wataalamu wa Hospitali wa KCMC.

Katika siku ya pili wadau pamoja na Waziri Mkuu Majaliwa, watashiriki matembezi ya hisani ikiwa ni kuunga mkono tamko la waziri mkuu.

Akizungumzia taarifa za uwekezaji na hesabu za mfuko, alisema hadi sasa unathamani ya rasilimali ya Sh trilioni 1.17.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles