28.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mhagama ateta na Wenyeviti CCM wa Mashina Peramiho

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jensita Mhagama(mb) Peramiho, amewapongeza Wenyeviti wa Mashina na Kata kwa kazi nzuri wanayofanya ya kulinda na kukipigania Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pongezi hizo amezitoa alipokutana na kufanya vikao na Wenyeviti wa Mashina wa Kata ya Muhukuru Lilahi, Mpitimbi Ndongosi Litapwasi katika ziara yake aliyoifanya Februari 26, 2024 jimboni Peramiho Halmashauri ya Songea vijijini mkoani Ruvuma.

Amesema Wenyeviti wa Mashina ndiyo wanaobeba na kusimamia ajenda ya Chama Cha Mapinduzi na Viongozi wataendelea kuchapa kazi katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.

“Tunapojiandaa kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa, hatuna mashaka kwa sababu viongozi wa mashina wameshaamua Jimbo hili la Peramiho ni la Chama Cha Mapinduzi,” alihimiza.

Aidha, amesema kuwa wanafanya hivyo kwa nia ya kuendelea kumshukuru Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi kubwa za ujenzi wa miradi ya Maendeleo katika Sekta ya Afya, Barabara, Nishati, Elimu na Utoaji wa pembejeo.

“Tuna kila sababu ya kujivunia mambo mazuri yaliyofanywa na serikali, ili kuimarisha uongozi wa Chama Cha Mapinduzi na tukumbuke kuwa Menyekiti wa Chama wa Taifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anawajali nasi hatuna budi kuwajali na kuwaheshimu Wenyeviti wa Mashina,” alieleza Waziri Mhagama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini, Thomas Masolwa amemshukuru, Jenista Mhagama kwa kuwathamini na kutembelea Mabalozi wa Chama cha Mapinduzi katika ngazi ya Shina.

Amesema Mabalozi ni watu muhimu kwa uhai na utendaji wa kazi wa Chama Cha Mapinduzi kwa sababu ndio wanaopokea kero za wananchi.

“Niwaombe Mabalozi muendele kufanya kazi ya kusajili wanachama wapya Ile wale wasio wanachama wawe wanachama wa Chama Cha Mapinduzi,” alisema.

Ameongeza kuwa katika kujenga Chama, Mabalozi wahamasishe wanachama katika kulipa ada ya chama na kufanya mikutano na wananchi kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Awali, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilayani humo, Juma Nambaila amemshukuru nakumpongeza, Jenista kwa kutelekeza maelekezo ya chama kivitendo kwa kupitia ofisi za Chama.
“Tayari kupokea na kutekeleza maelekezo ya Serikali pamoja na maelekezo ya chama ” alibainisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles