25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI: KASI YA KUDHIBITI UKIMWI HAINIRIDHISHI

Ramadhan Hassan, Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameagiza nusu ya vituo 3,400 vinavyotoa huduma ya kupima Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa wajawazito kutumika kupima na kuhudumia watu waishio VVU.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Ummy ameonyesha kutoridhishwa kasi ya kudhibiti ugonjwa wa ukimwi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Mei 9, Jijini hapa kwenye maadhimisho ya miaka 30 ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) yaliyokwenda sambamba na Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Nne wa Kudhibiti Ukimwi.

“Haipendezi kuona asilimia 48 ya Watanzania wanaohisiwa kuwa na VVU hawajui hali zao, takwimu zilizopo zinaonesha maambukizi ya ukimwi yamepungua kwa asilimi 0.4 kwa kipindi cha miaka mitano kutoka asilimia 5.1 mwaka 2011/2012 hadi asilimia 4.7 kwa mwaka 2016/2017.

“Kwa sasa nchi bado inakabiliwa na kazi kubwa ya kufikisha malengo sifuri katika kupambana na magonjwa hatari ifikapo mwaka 2010 na kusisitiza haja ya sekta zote kushiriki katika kutokomeza ugonjwa huo,” amesema.

Naye, Mkurugenzi wa Ofisi ya Afya ya USAID, Laurel Fain amesema unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya wagonjwa wa Ukimwi ni mambo muhimu ambayo serikali inapaswa kuyaangalia katika kupambana na ugonjwa huo ambapo amehimiza serikali kuweka kipaumbele zaidi kwa zaidi vijana na wanawake kama lengo kuondoa ugonjwa huo ifikapo 2030.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles