28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI ATOBOA CHANZO MIGOGORO ARDHI

Na SAM BAHARI -SHINYANGA

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,   Angelina Mabula amesema ukiukaji wa sheria, sera na taratibu zinazosimamia ugawaji na umiliki wa hati za ardhi ndiyo chanzo cha kukithiri   migogoro ya ardhi nchini.

Akizungumza na MTANZANIA   kwa njia ya simu,   Mabula alisema imebainika kuwa migogoro mingi ya viwanja husababishwa kwa makusudi na watumishi wa idara ya ardhi katika halmashauri.

Alisema baadhi ya maofisa ardhi wateule katika halmashauri za wilaya, manispaa na jiji hukiuka kwa makusudi taratibu za kutunza  majalada ya wateja wao kwa lengo la kuwanyang’anya na kuwapora viwanja vyao baadaye hivyo kuzua migogoro.

Waziri alisema majalada ya mengi ya wateja ni mapya na inaonekana yanaanzishwa bila kuwa na barua za maombi ya wateja wanaohitaji kupewa na kumilikishwa kiwanja na hayana taratibu za kuandikiwa madokezo yanayoonyesha mwenendo wa jalada.

“Licha ya majalada kukosa barua za waliomba na kugawiwa viwanja lakini pia utaratibu mbovu wa kutoandika dokezo kuonyesha mwenendo wa jalada husababisha kutokujua kwa urahisi jalada liko wapi kwa wakati huo.

“Kutokana na ukiukwaji wa sheria na upotoshaji wa sera za ardhi ambao umekuwa ukifanywa na wafanyakazi wa idara ya ardhi  kwa makusudi umekuwa ukisababisha uporaji wa viwanja na hati miliki kwa kiwanja kimoja kwa watu wawili,” alisema.

Mabula alisema ofisa ardhi wateule ambao wataendelea na mpango na utaratibu unaokinzana na sera za ardhi watafukuzwa kazi kwa lengo la kuwanusuru wananchi wengi wanaoporwa viwanja vyao na kupoteza haki zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles