22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

WAZIRI ATAKA MFUMO WA KUKAGUA MIZIGO KABLA YA SIKU NNE


Na MANENO SELANYIKA-DAR ES SALAAM   |

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amezitaka Mamlaka ya Bandari (TPA), Reli (TRL) na Kampuni ya Kupakua na Kupakia Makontena Bandarini (TICS) kukamilisha kuunganisha mfumo wa kukagua mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam kabla ya Ijumaa wiki hii.

Waziri Mbarawa alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana katika ziara ya siku moja ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya mashine hizo zilizofungwa katika bandari hiyo.

“Hadi Ijumaa watendaji wa TPA, TRL na TICS waniletee ‘Implementation plan’ yao ya kuunganisha huu mfumo uweze kufanya kazi kwa pamoja na ili kama watakuwapo wajanja wajanja wanaoendelea kurudisha nyuma katika sekta hii muhimu kwa ukuaji wa uchumi wetu,” alisema.

Alisema serikali ina jukumu la kuandaa wataalamu wazuri wenye uwezo, weledi na wazalendo walio na ujuzi wa kusoma ‘scaner’ hizo za kisasa ambazo zitatumika wakati wa kupakia mizigo ama kwenye treni au katika gari kabla ya kusafirisha.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko, alisema atatekeleza agizo la waziri kabla ya siku hiyo kuhakikisha mapato ya nchi yanaonekana na kuwanufaisha watu wote.

“Kwa sasa scaner zimefikia 11 kwa mantiki hiyo TPA na TRL tumejipanga hivyo tutakaa pamoja na watendaji wangu tuunganishe hizo cable kisha kumpatia Waziri taarifa ya namna mfumo huo utakavyofanya kazi kwenye sekta hizo,” alisema Kakoko.

Awali, Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, Ben Asubisye, alisema kuwapo mashine hizo kutasaidia kuongeza na kukusanya mapato ya nchi na kuwataka watendaji kuzitunza kwa sababu ni baraka kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa.

“Ni lazima tuone mradi huu unafanikiwa kwa sababu serikali yetu ime – invest fedha nyingi, hatutegemei awamu hii mtu atuambie ameigiza vitenge kumbe amebeba ‘toilet paper’ kwa nia ya kukwepa kodi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles