22.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Wazinzi kupigwa mawe hadi kufa Brunei

BANDAR SERI BEGAWAN, BRUNEI

SHERIA mpya kali za Kiislamu kuhusu uhalifu zimeanza kutekelezwa jana nchini Brunei zikitoa adhabu watu wanaoshiriki uasherati na ngono ya jinsia moja.

Adhabu hizo zinazohusisha kuwapiga mawe hadi kufa watakaopatikana na hatia, zimezusha shutuma kutoka ndani na nje ya taifa hilo dogo la kusini mashariki mwa Asia.

Sultan Hassanal Bolkiah aliidhinisha sheria hiyo mwaka 2014 ili kuimarisha ushawishi wa Uislamu katika taifa hilo la kifalme lenye utajiri wa mafuta.

Brunei ina karibu watu 430,000 ambao theluthi mbili ni Waislamu.

Hata kabla ya 2014, ushoga tayari ulikuwa ukitolewa adhabu ya kifungo cha hadi miaka 10 jela.

Chini ya sheria mpya ambazo zinatumika hadi kwa watoto na raia wa kigeni, hata kama wao si Waislamu, watakaopatikana na hatia ya kufanya ngono ya watu jinsia moja hupigwa mawe hadi kufa au kuchapwa mijeledi.

Wakati wazinzi pia wakikabiliwa na adhabu kama hiyo, wezi wao wakikutwa na hatia watakatwa mkono wa kulia kwa kosa la kwanza na mguu wa kushoto kwa kosa la pili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles