24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi watakiwa kuwaangalia watoto walihitimu elimu msingi

Na MWANDISHI WETU

 WAZAZI na walezi ambao watoto wao wamehitimu elimu ya msingi wametakiwa kuweka uangalizi kwa watoto wao ili kutojihusisha na mambo yoyote ya uhalifu wanavyosubiri matokeo.

Hayo yalisemwa juzi na Ofisa Elimu Kata ya Mgulani, Glory Temba, wakati akizungumza na wanafunzi na wazazi wakati wa mahafali 16 ya kuhitimu darasa la saba juzi, jijini Dar es Salaam, katika Shule ya Msingi Taifa.

 Alisema wazazi wanatakiwa kuweka uangalizi kwa watoto wao ili kutojihusisha na masuala ya uhalifu kwani umri wao bado wanahitajika kuendelea na masoma.

 “Wazazi na walezi ni jukumu lenu kuhakikisha watoto wenu hawajihusishi na masuala yoyote ya makundi ya uhalifu kwani umri wao bado ni mdogo na wanatakiwa kuzingatia masomo” alisema.

 Alisema watoto wanatakiwa kusimamia na kuhakikisha wanafatiliwa na kuelekeza nguvu zao kwenye masuala ya masomo.

 “Kwanza watoto ndio kwanza safari inaanza hivyo tunatakiwa kuwawekea misingi mizuri ya kufikilia masomo yao na wala sio mambo mengine” alisema.

 Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Juliana Lubuva, alisema vijana hao wamehitimu kipindi ambacho nchi ipo kwenye uchaguzi hivyo usimamizi ni muhimu.

 Alisema kupitia uangalizi wa wazazi utasaidia kufikia malengo yao pasipo kuharibu ndoto zao.

 “Umri wao in mdogo japo wanaonekana na mambo makubwa hivyo usimamizi ni jambo la msingi na la lazima ili kufikia ndoto zao” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles