26.7 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

wazazi wanavyoharibu maisha ya watoto

Na Markus Mpangala

ROSA Mistika ni miongoni mwa vitabu vilivyotikisa anga za fasihi kwa muda mrefu tangu kuingizwa sokoni. Kitabu hiki kimeandikwa na Euphrase Kezila habi, nguliwa fasihi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Chapa ya kwanza ya kitabu hiki ilikuwa ya mwaka 1971 na baadaye toleo jipya lilichapwa mwaka 2015. kitabu hiki kimepewa nambari ISBN 9966-44-673-7  na kuchapwa na Dar es Salaam UniversityPress. Kitabu hiki kinapatikana katika duka la vitabu la TPH Bookshop jijiniDar es Salaam.

Mandhari ya kitabu hiki ni kanda ya ziwa, yaani Mwanza yalikokuwa makazi ya mhusika mkuu Rosa Mistika, pamoja na Morogoro na Dar es Salaam. Masimulizi ya kitabu hiki yanapatikana kwenye miji midogo ya Misungwi, Ukerewe, Namagondo na mengineyo.

Maudhui ya kazi hii yana mwonyesha Rosa Mistika ambaye amezaliwa katika familia yawatoto wa kike. Anachorwa kuishi chini ya baba mzazi Zakaria ambaye anaami ni kuzaa watoto wa kike ni hasara.

Makuziya Rosa yaliyojaa vitisho na vipigo yaliambatana na nduguze Stella, Flora naHonorata. Watoto hawa wanaonyeshwa kukulia kwa baba mlevi ambaye hajali maisha ya familia yake. Zakaria amekuwa mtu mwenye kutumia ukali na kukaripia kila wakati na kuwafanya watoto wake wakimwogopa.

Mwandishi anatuonyesha sura tofauti ya mke wa Zakaria, yaani Regina ambaye wakati wote alikuwa akiwaelimisha watoto wake kwa upole na unyenyekevu njia za kuishisalama na kuepuka kuharibikiwa maisha.

Rosa Mistika anasoma kwa shida. Maisha ya nyumbani kwao ni tatizo. Anakulia kwenye dhiki na fadhaa. Anavumilia kero za baba yake ambaye amekuwa mwiba mchungu na mlevi kupindukia asiyejali familia yake.

Zakaria anaonyeshwa namna alivyochukua fedha za karo za Rosa na kwenda kunywea pombe. Kimsingi Rosa anaumbwa kama mhusika mkuu ambaye anakabiliwa na matatizo makuu matatu; dhiki na uongozi mbovu wa baba yake nyumbani, mabadiliko ya mwili na utambuzi wa ukuaji, pamoja na kukosa mwongozo wa elimu ya rika kwake na wadogo zake.

La mwisho, ni namna anavyoweza kupambana na umasikini ulioizingira familia yaketangu mawio hadi machweo. Ni sababu hizo zinamfanya Rosta ajitumbukize kwenyetabia mbaya.

Tangu alipopigwa na baba yake na kukatazwa kuwa karibu na wavulana, Rosa aliwaogopa.Lakini akiwa shuleni alijikuta akitoroka na kwenda mijini kukata kiu ya kitualichohitaji, kujitosheleza.

Rosa anaonyeshwa kuwa hakuwezi kujitosheleza maishani, alihitaji mambo yanayohitajika kwa mwanadamu yeyeto maishani.

Lichaya misukosuko ya kufukuzwa shule na Sista John kutokana na kutoroka shule ni mara kadhaa kwenda kulala na wanaume; vijana na wazee, aliruhusiwa kufanyamtihani wa mwisho (Cambridge). Rosa anaonyeshwa kufaulu mitihani na kwenda Chuocha Ualimu Morogoro.

Huko nako anajikuta akipata misukosuko iliyomlazimu kujihusisha kimapenzi na mkuu wa chuo, kuendekeza tabia mbovu zilizotokana na mpangilio mbovu wa malezi nyumbani.

Kimsingi Rosa anaonyeshwa kama msichana asiyejali lolote na alifanya ufuska hadi alipochoka. Changamoto yake ni pale alipohitaji kuolewa na Charles, ambapo alijiokuta akidanganya kuwa yeye ni bikira.

Dhamira kuu zilizowekwa ndani ya simulizi hii; umasikini wa familia ya Mzee Zakaria ulikuwa kikwazo cha ufanisi. Changamoto iliyojitokeza ni pale Rosa alipochaguliwa kuendelea na masomo huku familia yake ikiwa imezingirwa naumasikini wa kutupwa.

“Zakaria alisema kwamba hakuwa na pesa. Kwahiyo, mpango ulifanywa wa kuuza ng’ombemmoja. Regina alivyokuwa na nia ya kuendeleza binti zake katika masomo hakupinga. Zakaria alipokwenda kunywa pombe aliwatangazia watu kwamba alikuwana ng’ombe jike wa kuuzwa,” (uk.9). Hivyo ndivyo Rosa alivyokwenda shuleni.

Katika suala la malezi mabovu, mwandishi anamuumba Zakaria kama mzazi asiyekuwa nausikivu wala mfumo mzuri wa malezi. Mwandishi anaonya mtindo wa kulea watotokwa vitisho na hofu hali ambayo huwajengea hisia hasi na kubaribu maisha yao yabaadaye. Rosa Mistika alikulia kwenye vipigo tu.

“Rosa alipigwa tena na tena, makofi yalikwenda mfululizo hata damu ikamtoka puani namdomoni. Alilia, ‘Baba nihurumie, sitarudia tena nimekoma.” Rosa alinyang’anywashuka. Chupi ilimwokoa lakini matiti yalikuwa nje. Ole wao watakaoyaona matitiya binti zao! Regina machozi yali mteremka mashavuni. Alilia kwa sauti. Watotowalipomwona analia nao pia walianza kulia. Zakaria hakujali,”(6-7).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles