24.8 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali itoe ufafanuzi wa kina wimbo, bendera ya taifa

TANGU Tanganyika ilipojitawala kutoka kwenye makucha ya wakoloni, kumekuwapo na mambo ya kujivunia na yameunganisha Watanzania kuwa kitu kimoja.

Mojawapo ni wimbo wa taifa ambao ni kielelezo tosha cha kulitambulisha taifa sehemu yoyote duniani.

Kila mmoja wetu anautambua na kuuheshimu  wimbo huo kutokana na umuhimu wake kwa taifa letu.

Katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuna taarifa kuwa Serikali imepiga marufuku wimbo huo kuimbwa kwenye taasisi za elimu.

Taarifa za kuzuiliwa kwa wimbo huu, zilianza kusambaa juzi kwa barua iliyoandikwa Novemba 23, mwaka huu yenye kumbukumbu CHA-56/193/02/16 ambayo inasema wizara imepokea  maelekezo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu matumizi sahihi ya bendera ya taifa, nembo ya taifa na wimbo wa taifa.

Barua hiyo ambayo imetoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaelekezwa kwa wakuu wa vyuo vya ualimu, wakuu wa vyuo vya maendeleo ya jamii, wakuu wa vyuo vikuu vishiriki na taasisi zilizopo chini ya wizara hii kuzingatia matumizi sahihi ya tunu zataifa.

Barua hiyo inasema endapo kuna sherehe ambazo hazitambuliki kitaifa, taasisi inapaswa kuomba kibali kwa waziri mwenye dhamana kuhusu matumizi ya tunu hizo.

 Sawa hatukatai kuhusu uamuzi huo, lakini jambo hili linahitaji ufafanuzi wa kina kwa walengwa.

Lakini pia barua hii, imesema bendera ya taifa ina rangi nne ambazo ni dhahabu, nyeusi, kijani na bluu nakwamba ni makosa makubwa kutumia rangi ya njano.

Sisi wa Mtanzania tumeshangazwa na uamuzi wa kuzuia wimbo wa taifa kupigwa taasisi za elimu, tukiaminikwanza kwa namna moja au nyingine, lazima utaathiri watoto au vijana ambao wamezoa kuuimba kila siku.

Kila mmoja wetu anatambua namna ambavyo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanavyoimba wimbo huu kila siku asubuhi kabla ya kuingia darasani.

Katika hili tunasema lazima Serikali ije na ufafanuzi wa kina kuhusu katazo hilo ambao utakata kiu yavijana.

Tunakubalia na na Serikali kuwa wimbo huu hauwezi kuimbwa kila sehemu, lakini kwa taasisi za elimu bado unapaswa kuendelea kuimbwa maana huko ndiko watoto wanakoanza kujifunza uzalendo kwa taifa letu.

  Jambola pili lililotushangaza ni kauli ya Serikali kusema kuwa katika bendera ya taifahakuna rangi ya njano. Hili pia linahitaji ufafanuzi wa kina.

Kwa miaka 57 ya uhuru wa Tanganyika watoto wetu wanasoma shuleni wakitambulishwa rangi hizo kuunda bendera ya taifa, sasa iweje mabadiliko haya yaje kimya kimya?

Sisi MTANZANIA, tunasema kuna vitu ambayo wakati mwingine havipaswi kufanyiwa majaribio.

Tunataka kujua sababu za msingi za mabadiliko haya ambayo yanaonekana hayakushirikisha watu wengi, zaidi ya kutolewa maagizo na mamlaka husika.

Tunamalizia kwa kusema tusiwatese Watanzania, vitu hivi bado vinahitajika kutumika katika taasisi za elimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles