28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Wazabuni watatu kuchuana ujenzi mradi wa mwendokasi Kibaha-Morogoro

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Serikali imepokea zabuni tatu za utekelezaji wa mradi wa barabara za mwendokasi kuanzia Kibaha hadi Morogoro ambapo awamu ya kwanza utaanzia Kibaha hadi Chalinze yenye urefu wa kilomita 78.9.

Akizungumza leo Februari 6,2024 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Ubia Nchini (PPP), David Kafulila wakati akifungua tenda za wazabuni hao amesema jumla ya makampuni tisa yaliwasilisha nyaraka zao lakini anahitajika mmoja.

Amesema Serikali inajenga barabara ya Kibaha , Mlandizi, Chalinze na Morogoro ya kilomita 205 kwa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi ambapo PPP imegawa barabara hiyo katika sehemu mbili.

“Sehemu hizi mbili, sehemu ya kwanza ni Kibaha , Mlandizi, na Chalinze kilomita 78.9 na sehemu ya pili Chalinze hadi Morogoro kilomita 126.1 na tayari upembuzi yakinifu sehemu ya kwanza ulifanywa na Kampuni ya kishauri ya Cheli Engineering Co.Ltd kutoka Korea.

” Kazi ya upembuzi yakinifu ilikamilika Februari mwaka jana na kazi ya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kipande cha pili inaendelea, ” amesema Kafulila.

Amesema ujenzi huo utasaidia kupunguza muda wa kusafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro, hivyo kukuza uchumi kutokana na watu kufika haraka wanapokwenda.

Amesema pia mradi huo utawezesha upatikanaji wa ujuzi, kiufundi, kifedha, kiteknolojia na kimenejimenti kutoka sekta binafsi.

Kwa upande wake Meneja wa Miradi ya Ubia Kati ya Serikali na Sekta Binafsi TANROAD, Mhandisi Kitainda Michael amesema serikali ilikaribisha wawekezaji waliokuwa na nia ya kujenga na kuendeleza sehemu ya Kibaha hadi Chalinze kilomita 78.9 kwa uratibu wa PPP.

“Kwa ajili ya kuwachambua na kuweza kuwatumia nyaraka za zabuni wale watakaokuwa wamekidhi vigezo ili waweze kuandaa zabuni zao na kuziwasilisha TANROAD kwa kufanya usanifu wa kina, kujenga, kugharamia ujenzi, kuendesha, kukarabati pamoja na kurejesha kwa Serikali,” amesema Mhandisi Michael.

Amesema muda wa ujenzi unakadiriwa kwa muda wa miaka mitatu na mwekezaji kuendesha mradi ni miaka 30 ambapo baada mda huo mradi utarudishwa kwa serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles