24.8 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mashujaa wazitaka pointi tatu kwa Yanga

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Kueleke mchezo wao na Yanga, Kocha Mkuu wa Mashujaa FC, Mohammed Bares amesema wamejipanga kupata pointi tatu licha ya kwamba wanafahamu ugumu wa mechi hiyo.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utarajia kupigwa kesho Februari 8, 2024 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 7, 2024 jijini Dar es Salaam, Bares amesema wametoka kucheza mechi ngumu dhidi ya Simba wanaingia tena kwenye mechi ngumu lakini wamejipanga kuidhibiti Yanga.

“Ni mchezo mkubwa lakini kwenye mpira si mchezo mkubwa ni kujipanga tu na sisi tumejipanga kuidhibiti Yanga kwa sababu tunajua ina wachezaji wanaoweza kuamua matokeo,” amesema Bares.

Kwa upande wake mchezaji wa timu hiyo, Baraka Mtuwi amesema kwa kipindi hiki kila mchezo kwao wanacheza kama fainali na kuahidi kuwa hawatawaangusha mashabiki wao.

Mashujaa iliyoanza msimu huu kwa kasi hadi kukaa kwenye nafasi nne za juu mwanzoni mwa ligi hiyo, kwa sasa inashika nafasi ya 15 na alama tisa ikicheza michezo 13.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles