30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

WAWINDAJI HARAMU 570 WAKAMATWA SERENGETI

NA TIMOTHY ITEMBE,

WAWINDAJI haramu 570 wamekamatwa katika Hifadhi ya Serengeti kwa miezi sita mwaka jana kuanzia Julai hadi Desemba.

Hayo yalielezwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa, James Mbugi ambaye pia ni meneja ujirani mwema wa shirika hilo .

Alikuwa akikabidhi mradi wa bwawa la maji katika vijiji vya Gibaso na Karagatonga vya Kata ya Kwihacha uliogharimu zaidi ya Sh milioni 74.

Alisema wananchi pia wamechangia nguvu  zaidi ya Sh milioni 18 ili kutowategemea wahisani tu.

Mbugi alisema majangili hao wamefikishwa mahakamani na kufunguliwa mashitaka yanayowakabili.

Diwani Kata ya Kwihacha, Mstapha Masyani, alilipongeza shirika hilo kwa kuwachimbia bwawa na kuwapunguzia wafugaji kutembea mwendo mrefu kwenda kutafuta maji ya kunywesha mifugo yao.

 Masyani alitumia nafasi hiyo kulitaka shirika hilo kuongeza birika la kunyweshea mifugo.

Alisema lililopo halitoshi kwa kuzingatia kuwa mifugo ndani ya kata hiyo ni mingi.

Vilevile aliomba wahisani hao kuwajengea birika la kunyweshea mbuzi na kondoo kwa sababu la kunyweshea ng’ombe halikidhi mahitaji.

Mkazi wa Kijiji cha Karagatonga, Lucus Manga (60) alisema  wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kwenda mto  kilomita tano  kwenda kuchota maji na kunywesha mifugo.

Alisema jambo hilo lilikuwa ni kero kwao hivyo akataka iundwe kamati ya maji ya kusimamia mradi huo.

Mkuu wa Wilaya Tarime, Glorius Luoga aliwataka wanajamii kuheshimu mradi huo na kuutumia vema uweze kudumu kwa manufaa yao.
 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles