25.3 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

TRA YAKUSANYA SH TRILIONI 8.42 KWA MIEZI SITA

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya Sh trilioni 8.41 kuanzia Julai mwaka jana hadi Januari mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo, inaonesha makusanyo ya Januari mwaka huu ni Sh trilioni 1.14.

Kayombo alisema pamoja na juhudi za kukusanya kodi mbalimbali, hivi sasa wameelekeza nguvu katika kukusanya kodi ya majengo kwa kutoa ankara kwa wamiliki wa majengo katika mikoa mbalimbali.

“Wamiliki wa majengo wanakumbushwa kwamba kodi ya majengo inakusanywa na TRA kuanzia Julai mwaka jana, hivyo tunawaomba watoe ushirikiano kwa kulipia ankara zao kwa wakati,” alisema Kayombo.

Kuhusu zoezi la uhakiki wa Namba ya Mlipakodi (TIN), alisema kuna mafanikio makubwa na kwamba wananchi wa mikoa ya Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Tanga na Pwani waitikie wito huo mapema kuepuka usumbufu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles