20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

WAWEKEZAJI WAZAWA WATISHIA KUFUNGA VIWANDA

 

|Peter Fabian, MwanzaWawekezaji wazalendo wanaomiliki viwanda vya kutengeneza bidhaa za sukari wametishia kufunga viwanda vyao endapo serikali na taasisi zake haitachukua hatua za kuthibiti uingizwaji wa bidhaa kwa njia za panya maeneo ya mipakani.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza juzi, Wakurugenzi hao, Lameck Airo wa Kampuni La Kairo Industries Gourp Ltd na Fayaz Rashid wa Kampuni ya Furaha Nyanza Ltd  ambao wamewekeza viwanda vya kutengeneza bidha mbalimbali zikiwamo pipi, jojo, biskuti na mifuko ya sandarusi.

Airo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rorya mkoani Mara (CCM), amesema hali ya uzalishaji kwenye kiwanda chake cha kutengeneza pipi, jojo, mifuko ya sandarusi umekuwa akikosa soko kutokana na bidhaa kama anazozalisha kuingizwa kwa njia za panya mipakani na kuuzwa bei ya chini zaidi ikilinganishwa na wao.

“Bidhaa zetu tunalipa umeme, kodi na ushuru wa malighafi lakini bado tunawalipa mishahara wafanyakazi, kutokana na bidhaa zetu sokoni kushindwa kununuliwa na wafanyabiashara wakikimbilia bidhaa zinazoingizwa kinyemela kwa njia za magendo ambazo zinauzwa bei ya chini,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,102FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles