28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

WAWA NJE, KAGERE NJIAPANDA SIMBA

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

SIMBA wanatarajia kushuka dimbani leo kukabiliana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, huku wakimkosa beki wao, Pascal Wawa.

Wakati Wawa akiukosa mchezo huo wa raundi ya pili, straika hatari wa Wekundu wa Msimbazi hao, Meddie Kagere, yupo katika hatihati kuwapo kikosini leo.

Simba itaikaribisha Mtibwa Sugar ikiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa kwanza wa ligi hiyo, Agosti 29, mwaka huu.

Kwa upande wao, Mtibwa Sugar wanatarajiwa kuishukia Simba wakiwa na hasira ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Lipuli kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.

Timu hizo zilipokutana msimu uliopita, mzunguko wa kwanza Simba walipata ushindi wa mabao 3-0, kabla ya kutoka suluhu waliporudiana mjini Morogoro.

Simba imepania kuendeleza ushindi katika mechi zake za Ligi Kuu ili kutetea taji lao kwa mara nyingine baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, alisema kuwa wanahitaji ushindi kwa kila mchezo, kwani wapinzani wao huwa wanapania mno wanapokutana na timu yao.

“Tutacheza lakini tutawakosa baadhi wa wachezaji, akiwepo Wawa ambaye bado anasikia maumivu ya nyama za paja kwa mbali pale anapocheza, lakini pia Kagere anatarajia kuingia leo (jana), ila nitaangalia kama nitaweza kumtumia,” alisema.

Kocha msaidizi wa Mtibwa Sugar, Patrick Mwangata, alisema hawatakuwa wanyonge mbele ya Simba kwani mipango yao ni kupata pointi tatu muhimu.

“Tulipoteza mchezo wa kwanza, hatutakuwa tayari kupoteza tena kwani tunahitaji kupata ushindi ili tujiweke katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles