Molinga apewa mabao 15

0
881

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa Yanga, David Molinga, ametabiriwa kufunga mabao kuanzia 15 hadi 20 msimu huu, ikiwa ni baada ya kuanza majukumu yake kwa kusuasua ndani ya klabu hiyo tangu aliposajiliwa hivi karibuni.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, alisema Molinga raia wa DR Congo, lazima afunge mabao 15 na kuendelea msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezaji huyo alitua Yanga katika dirisha la usajili lililopita akitokea FC Lupopo ya DR Congo na kwamba hadi sasa hajafunga bao lolote Ligi Kuu Bara.

Mchezaji huyo amepachika mabao matatu katika mechi za kirafiki, dhidi ya Pamba FC na Toto Africans zote za Mwanza.

Akimzungumzia mchezaji huyo Zahera alisema Molinga ni mchezaji mzuri kuliko straika wao wa zamani, Herieter Makambo waliyemuuza Horoya AC ya Guinea.

“Molinga ni mchezaji mzuri kuliko alivyokuwa Makambo kwani waliwahi kucheza ligi ya Congo (DRC) na Molinga alimaliza na mabao 15 huku Makambo akifunga saba. Subirini mtaona na endapo asipofunga, basi natoa dola 1,000 (sh milioni mbili),” alisema.

Alisema mchezaji huyo anatakiwa kupewa muda zaidi akiamini mashabiki watamkubali tu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here